Kikao cha siri - sehemu 2
Sehemu ya pili ya simulizi ya ucheri na mwajiri wake, jinsi alivyopelekeshwa kimapenzi kazini na kujikuta akiwa kwenye matatizo mengi na mikasa mingi
Simulizi ya ucheri na mwajiri wake, jinsi alivyopelekeshwa kimapenzi kazini na kujikuta akiwa kwenye matatizo mengi na mikasa mingi
Sikuwahi furahia maisha yangu tena baada ya fumanizi lile, tena ikiwa ni eneo nililoliheshimu siku zote na kujiambia kua sitowahi kaa nipavunjie heshima eneo, tena na watu wanaoniheshimu sasa. daaah..
lakini huyu mwanamke alinifanya nivunje maagano yangu yote, ila ni mungu tu mpaka sasa naendelea vizuri na afya ipo njema kabisa japokua sehemu kubwa ya maisha yangu imeharibika kisa yeye.
Naitwa Ucheri Jango, ni kijana mwenye umri wa miaka 36, niliyozaliwa mikoa ya kusini sehemu zenye ukanda baridi, kijana mrefu mweusi mwenye malengo makubwa ya kuja kuikomboa familia yake ambayo imeishi maisha ya tabu nyingi na shida nyingi..
nyumbani kwetu mimi ndo nilikua mtoto wa kiume pekee kati ya watoto 6, hivyo kazi nyingi ilikua nikitumwa sana mimi na kwenda shambani sana huku dada zangu tukisaidiana nao hapa na pale.
miaka hiyo maisha niliyaona ya kawaida tu, kwakua ni utoto ulinijaa kichwani, ila nakumbuka kipindi nakua, dada zangu wawili waliozeshwa siku moja na walikua wakilia sana, sikuelewa lile tukio mapema ila baadae mama alikuja nielekeza kua dada zangu wanaozeshwa kwa wazee wanaowajua wao, na tayari walishapokea mahari kubwa ambayo ingenisomesha mimi na dada zangu wengine.
niliona kawaida sikujali sana, na siku zilienda na tukaanza shule huko huko kijijini. hakika maisha yalienda kwa haraka sana na tuliishi kawaida tu bila ya kua na mawazo mengi kichwani.
nilifanikiwa kuhitimu kidato cha nne na kisha nikaenda kusomea astashahada kwakua familia yangu haikua na uwezo sana na nilitamani niwahi kupata kazi ili niwasaidie.
wale dada zangu wengine, watatu waliacha masomo na kuolewa na walikua na maisha magumu sana tu, mara nyingi walikua wakilia pindi wanavyorudi nyumbani, lakini baba alishawaambia wasije rudisha mabegi kwakua aliwapambania wasome ila wao walikataa na kuolewa.
kwahiyo nilibaki mtoto pekee ambaye sikukata tamaa na masomo, na niliendelea kukomaa. nilivyomaliza elimu yangu ya astashahada, niliendelea na masomo huku nikifanya vibarua vya hapa na pale ili nisikose pesa za kula.
nilipambana hadi kufikia kuhitimu elimu ya shahada katika utawala wa mifumo ya fedha na rasilimali watu, nilifurahi sana kuhitimu na nikasema lazima nifanikiwe ili wazazi wangu waheshimike pamoja na familia yangu yote pamoja na yangu itakayokuja huko mbele.
haikua rahisi kupata kama nilivyofikiri, ilifika kipindi niliweka vyeti vyangu pembeni na kuanza kuosha magari ya watu mtaani ilimradi nisikose pesa.
nilipambana kwa muda wa miaka miwili huku nikiwa nimekosa matumaini ya kutimiza ndoto zile nilizozifikiria kipindi na hitimu elimu ya shahada.
siku moja nikiwa sina pesa wala hili wala lile, nikiwa kijiweni sehemu tunayooshea magari, nilisikia mlio wa tairi kupasuka barabarani na kuangalia ilikua gari RAV 4 nyeusi mpya na ilikua imekamata breki zote na kuserereka kisha ikasimama, sauti ilikua kubwa na watu wengi walishtuka lakini waliendelea na mambo yao.
kwa ukarimu wangu nikasogea pale kutaka kujua nini kimetokea, akashuka dada mmoja mweupe amevaa mini skirt nyekundu na blauzi ya rangi ya maziwa hivi inayoteleza huku amevalia miwani nzuri sana na mwenye shepu mashalaaah, nikamsalimia kisha nikamuuliza kama yuko salama, akanijibu yupo salama huku akikagua gari lake na kuzunguka zunguka akijaribu kupiga simu, lakini alionekana wote anaowapigia ni kama hawapokei simu zake, akawa kama anatafakari afanyaje.
kuona vile, nikamuuliza kama ana tairi la ziada ili nimsaidie kufunga, alivyosikia alijibu haraka kua analo na kwenda kufungua buti ya gari na kunionesha lilipo, kisha akawa anajiongelesha akinishukuru maana watu wake walikua hawapatikani.
basi mimi nikaingia kazini na kuanza kufungua tairi, lakini jua lilikua kali na niliona akihangaika kujizuia jua usoni, ndipo nikainuka na kumwambia aje kwenye kijiwe chetu cha kuoshea gari maana hakukua na mtu na kulikua na benchi lenye kivuli kwa juu, nikamuomba akae hapo huku nikimalizia kazi yake. alikubali.
kama baada ya dakika kumi na tano nilikua nimeshamaliza na kuja kumwambia, nikamkuta akiwa ananiangalia sana, nikamstua akashtuka kidogo, nikamwambia kua kazi yake tayari anaweza kwenda, kisha nikamwambia awe makini barabarani maana watu ni wengi na magari ni mengi.
yule dada aliinuka kisha akaniuliza tu jina langu, nikajibu kua ni ucheri, kisha akatabasamu na kuelekea kwenye gari yake, akafungua mlango wa dereva na kuinama hivi kama anachukua kitu ndani, mhhh hakika ni mrembo, mguu mweupeee, magoti mpaka yana dimpozi, yaani nilibaki kumtazama tu, nikijisemea tu pesa sina ndo ntamuweza!!.
yule dada akafunga mlango na kurudi nilipokua nimekaa kisha akanishukuru na kunyoosha mkono wake ukiwa na kiasi fulani cha pesa, niliikataa mwanzoni nikamwambia asijali maana nilikua namsaidia tu. ila yule alisisitiza kunipa basi nikaipokea kisha akaniambia kua atarudi tena siku nyingine kuosha gari, na kwenda zake kwenye gari na kuondoka.
nilibaki nikimuwaza tu, ile sauti yake, muonekano wake ulivyo mzuri, rangi yake, maumbile yake ya nyuma, miguu yake, uso wake, tembea yake yaani nilibaki mdomo wazi nikapiga na makofi nikisema “chaii wenye pesa wanafaidi..”.
Msimulizi wa simulizi nzuri na zenye kusisimua
Sehemu ya pili ya simulizi ya ucheri na mwajiri wake, jinsi alivyopelekeshwa kimapenzi kazini na kujikuta akiwa kwenye matatizo mengi na mikasa mingi
These cookies are essential for the website to function properly.
These cookies help us understand how visitors interact with the website.
These cookies are used to deliver personalized advertisements.